UJUMBE KUTOKA KWA BALOZI WA SWEDEN TANZANIA KWA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI MIKOA YOTE TANZANIA TAREHE 3 MEI 2021
Habari za leo,
Mimi kama Balozi wa Sweden ninafurahi kuwepo leo kusherekea uhuru wa habari na kujieleza. Sweden na
Tanzania ni marafiki wa siku nyingi, na wote tunatambua kwamba nguzo hii, sambamba na haki ya kupata
taarifa ni muhimu sana kwa jamii inayoheshimu Demokrasia na Haki za Binadamu.
Sweden inaamini kwamba maendeleo ya nchi yoyote ile yanapatikana kwa kupeana tarifa, kujadiliana kwa
uwazi, na kuwajibishana. Basi sisi tutaendelea kuungana na watanzania wote katika jitihada za kukuza na
kuendeleza uhuru wa habari na kujieleza nchini.
Asanteni sana kwa kunisikiliza
No comments:
Post a Comment