Robert Kakwesi,Tabora
Tabora. Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua,watu wake wamehamasika kwa kuunda vikundi vya wajasiriamali 826 vyenye wanachama 8,820 ambavyo vinahitaji mikopo kutoka asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya makundi maalum ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Kutokana na hamasa kubwa iliyopekea idadi kubwa ya vikundi,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Jerry Mwaga,anasema halmashauri inakabiliwa na changamoto kubwa kwani uwezo wake ni kutoa mikopo kwa vikundi 45 kwa mwaka.
Akizungumza wakati wa Utoaji Hundi yenye thamani ya Sh240milioni kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu 32,amesema sekta ya maendeleo ya Jamii ikutumika vizuri ,inaweza kuleta maendeleo Chanya na haraka kwa jamii.
"Fursa hii muhimu na adhimu ni lazima itumike vizuri kwa manufaa ya wahusika na jamii mzima kwa ujumla"Amesema
Mkurugenzi Mwaga pia amesema wanatoa hata vifaa kwa ajili ya wajasiriamali ambao 15 wamekabidhiwa pikipiki kwa ajili ya Biashara ya bodaboda huku watendaji 25 wakikabidhiwa pikipiki 25 kwa ajili ya utendaji kazi na kufanya zote 40 kuwa na thamani ya Sh69milioni.
Akikabidhi Hundi na pikipiki,mkuu wa mkoa wa Tabora,Dk Batilda Burian,amewahimiza wajasiriamali kurejesha mikopo kwa wakati ili na wengine na vikundi na wenyewe waweze kukopa.
Amewaasa kutofanya kiburi kwa kusubiri Hadi waanze kufuatwa au kutaka kupelekwa mahakamani ndio waanze kurejesha.
"Fursa hii mnayopata muitumie vizuri huku mkikumbuka na wengine wanasubiri mrejeshe ili nao wakope kamwe msisubiri mfuatwe au kutaka kupelekwa mahakamani ndio mrejeshe"Amesema.
Katika vikundi hivyo,vikundi 11 vya wanawake na vikundi 8 vya vijana ,vyote vikipata jumla ya Sh192milioni wakati vikundi 13 vya watu wenye ulemavu vikipata jumla ya Sh48milioni.
No comments:
Post a Comment